Swahili- Let the Journey begin!

 SHERIA NA NEEMA  (LAW AND GRACE)

MADONDOO      YA      MANDIKO      TAKATIFU          (SCRIPTURE REFERENCE)

NI KUSUDI GANI KUWA NA SHERIA? (WHAT IS THE PURPOSE OF THE LAW?)

  Waroma 3:19,20:-Hata hawawezi kuwa na kisingizio chochote na ulimwengu wote uko chini ya hukumu ya Mungu .Maana hakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwa mwadilifu mbele yake  Mungu kwa kushika sheria ,ni kuwaonyesha tu mtu kwamba ametenda dhambi.

Waroma 4:15:-Sheria imeshababisha ghadhabu;lakini kama hakuna sheria ,haiwezekani kuivunja.

Waroma 5:13,20:-Kabla ya sheria kuweko,dhambi ulikuweko ulimwenguni lakini dhambi haiwekwi kwa kumbukumbu bila sheria. ….Sheria ilitokea,ikashababisha kuongezeka kwa uhalifu.

Waroma7:5,7,9,13:-Tamaa mbaya zikichochewa na sheria …..lakini bila sheria ,mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani,maana nisingalijua nini hasa kutamani mabaya kama sheria isingalikuwa imesema “usitamani”,maana bila sheria dhambi ni kitu kilichokufa ….lakini amri ulipokuja ,dhambi ilifufuka …hivyo dhambi kwa njia ya ile amri ilijionyesha kikamilifu jinsi ilivyombaya mno.

1 Wakorintho 15:56:- Naye dhambi upata nguvu yake kutoka kwa sheria.

Wagalatia 3:19,24:-Ya nini basi,sheria?iliongezwa hapo ili {kuonyesha} uhalifu ni kitu gani….Basi hivyo sheria ilikuwaa kwa mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo ,ili kwa njia ya imani tufanywe kuwa watakatifu mbele yake mungu.

Wahebrania 10:1,3:-Kwa vile sheria ni kivuli tucha mamboneema yatakayokuja …..lakini dhabibu hizo hufanyika kila mwisho kuwakumbusha watu dhambi zao.

1 John 3:4:-Maana dhambi ni uvunjaji wa sheria.

 

Bauer ,Arndt , Gingrich, Danker 887A.

 

SHERIA HUTIMIZWA VIPI?  (HOW IS THE LAW FULFILLED?)

Mathayo 7;12:- Yote mnayotaka watu wawatendee ninyi ,watendeeni wao vivyo vivyo.Hii ndivyo maana ya sheria ya Musa na mafundisho ya manabii.

Mathayo 22:40:- Sheria yote ya Musa na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.

Luka 10;25,37:- Mfano wa Msamaria Mwema.

Waroma 8:3,4:-Mungu ametekeleza jambo ambalo sheria haikuongea kutekelezakwa sababu ya udhaifu wa binadamu .Mungu alituma mwanae…….kusudi matakwa ya sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi.

Waroma 13;8-10:- Ampendaye jirani yake yake ameitekeleza sheria.kwa maana [orodha ya sheria ama amri hizi] zimo katika hii sheria moja.” Mpende jirani yako nafsi unavyo jipenda mwenyewe”basi upendo ni utimilifu wa sheria.

Wagalatia 5:14:-Maana sheria  yote hutimizwa katika kushika amri hii moja .”Mpende jirani yako kama unavyo jipenda mwenyewe “.

Wagalatia 6:2:-Chukulianeni  mizigo yenu ,na hivyo mtatimiza sheia ya Kristo.

Yakobo 2:8:-Kama mnaitimiza ile sheria ya ufalme kama ilivyoandikwa katika maandiko Matakatifu.”Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”

Mathayo 5:17:-Msidhani kuwa nimekuja kutangua {sheria na mafundishoya manabii}.Sikuja kutangua bali ni kitimiza.

 

NANI HAYUKO CHINI YA MAMLAKA YA HUKUMU WA SHERIA?

(WHO IS NOT UNDER THE JURISDICTION OF THE LAW?)

Waroma 6;14:-Kwani hamko chini ya sheria bali chini ya neema.

Waroma 7:4,6:-Nyinyi pia mmekufa kuhusu sheria ….lakini sasa tumekuwa huru kutoka viungo vya sheria ….sasa tunatumikia kufuatwa na maisha mapya ya roho ,na  si kufuatana na hali ile ya kale ya sheria iliyoandikwa .

Waroma 10:4:-Kwa kuja kwake kristo ,sheria imefika kikomo chake.

Wagalatia 2:19:-Sheria enyewe iliniua,nipate kuishi kwa ajili ya Mungu.

Wagalatia 3:13:-Kristo alitukomboakutoka katika laana ya sheria.

Wagalatia 3:25:-Lakini vile ili imani imekwisha fika ,sisi hatuko tena chini  ya mlezi.[sheria ]

Wagalatia 5:18:-Kama mkiongozwa na Roho ,basi hamko tena chini ya sheria.

Waefeso 2;14,15:-Kwa mwili yake mwenyewe aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui.Aliondoa ile sheria pamoja na amri zake na kanuni zake.

Waebrania 7:8,9:-Basi ile amri ya zamani ilifutwa kwa sababu ilikuwa hafifu na isiyofaa kitu….mahali pakem pamewekwa tumaini lilibora zaidi {ambalo kwako tunaweza kukariba Mungu.

 

KUNA MAANA GANI KUWA CHINI YA NEEMA?

(WHAT DOES IT MEAN TO BE UNDER THE GRACE?)

Waroma 7:6:-Sasa tunatumikia kufuatana na maisha mapya ya Roho .

Waroma 14:14:-Katika kuungana na bwana Yesu ,nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi kwa asili yake.

Waroma 14:2,22:-Mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu ,heri mtu Yule ambaye ,katika kujiamulia la kufanya ,haipingi dhamiri yake.

1 Wakorintho 6:12:-Kwangu mimi kila kitu ni halali,lakini sio kila kitu inafaa.Nakubali kwamba kila kitu ni halali kwangu lakini sitaki kutawaliwa na kitu chochote.

1 Wakorintho 10:23:- Vitu vyote ni halali ,si vyote vifaavyo.vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga.

Wagalatia 5:1,13:-Kristo alitupa huru,akataka tubaki huru.mliitwa……..Mliitwa muwe watu huru.

Waebrania 8:12,13:-Nitawasamehe makosa yao ,wala sitakumbuka tena dhambi zao kwa kusema juu ya agano jipya Mungu aliichakaza lile la kwanza ;na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu,kitatoweka karibuni.

Waebrania  10;1,2,9,14,17:-Dhabihu ya Kristo huwafanya wawe wakamilifu wale wanaoabudu wametakaswa dhambi zao hata mwaka haziwezi kamwe kuwafanya wawe watakatifu ; hivyo Mungu alibakisha dhabihu za moja .Basi  kwa dhabihu yake moja ,amewafanya wawe wakamilifu milele .Sitakumbuka tena dhambi zao wala vitendo vyao vya uhalifu.

1 John 3:6,9:-Basi kila aishiye katika muungano na Kristo hatendi dhambi ,lakini kila mtu atendaye dhambi hatapata kamwe kumwona walakumjua Kristo.Kila aliye motto wa Mungu hatendi dhambi maana anayo hali ya kimungu ndani yake ,hawezi kutenda dhambi sababu yeye ni mtoto wa Mungu.

1 John 3:19,21,24:-Hivyo ndivyo  tuwezavyo kuwa na hakika kwamba sisi ni watu  wa ukweli ;na  hatutakuwa na wasiwasi mbele ya Mungu dhairi yetu haina lawama juu yetu ,basi tunaweza kuwa na uthabiti mbele ya Mungu na kupokea kwake chochote tunachoomba kwa njia ya Roho ambaye ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.

1John 5:18:-Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi.

 

NI MAJUKUMU GANI TULIYONAYO CHINI YA NEEMA?

(WHAT RESPONSIBILITIES DO WE HAVE UNDER  THE GRACE?)

Mathayo 22;37,39:-Mpende bwana Mungu wako kwa moyo wako wote ,kwa roho yako yote na kwa akili yako yote ….mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.

Waroma 14:19,22:-Kwa hivyo tuyatingazie daima mambo yenye kuleta amani na na yanayotusaidia  kujenga .Basi shikilia unachoamini kati yako na Mungu wako.

1 Wakorintho  8:9:-Lakini jihadharini huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.

1Wakorintho 9;19,22:-Kwa hivyo ingawa mimi sio mtumwa wa mtu yeyote ,nimejifanya  nimejifanya mtumwa wa kila mtu  ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.

1 Wakorintho10:24,31:- Mtu asitafute faida yake mwenyewe ,ila faida ya mwenzake ,kwa kila mfanyako iwe kwa kula au kunywa ,fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Wagalatia 5:13:-Uhuru huo usiwe kisingiziocha kutawaliwa na tama za kidunia ,ila mnapaswa kutumikia kwa upendo .Mwendo wenu na  uongozwe na roho nanyi hamtafuata tena  tama za kidunia.

Waebrania 10:24,25:-Jitahidi kushuhulikiana  kwa ajili ya kuongezaana bidii ya kupendana na kutenda mema.

1 John 3:22,23:-Na kupokea kwake chochote tunachoomba .Na kuzitii amri zake na kufanya yale yanayompendeza.na amri yake ndio hii  Kuamini mwanae Yesu Kristo na kupendana kama alivyotuamuru.

 

 

 

KUNA MIPAKA GANI KATIKA SHERIA?

(WHAT ARE THE LIMITATION OF THE LAW?)

Wagalatia 2:16,21:-Mtu hawezi kufanywa mwadilifu kwa kutii sheria ,bali tu kwa kuamini Yesu kristo.Kama mtu hufanywa mwadilifu kwa njia ya heria ,basi kristo alikufa bure.

Wagalatia3:11,12,21:-Ni dhahiri kwamba sheria haiwezi kuifanya mtu mwadilifu ,lakini sheria haitegemie imani …..kama kungalitoewa sheria ambayo ingeweza kuwapa uhai basi tungeweza kuwapa watu waadilifu kwa njia ya sheria.

Waebrania 7:19:-Maana sheria ya Musa haikuweza kukamilisha jambo lolote.

Waebrania 10:1:-Dhabibu zile zile za sheria zinzotolewa mwaka hata mwaka haiwezi kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu.

1 Wakorintho 15:56:-Dhambi hupata nguvu yake kwa sheria .

 

NI MADHARA NA ONYO GANI YA KURUDI KUWA CHINI YA SHERIA?

(WHAT ARE THE CONSEQUENCES AND WARNING OF GOING BACK UNDER THE LAW?)

Wagalatia 3:2,3,10:-Je,ulipokea roho wa Mungu kwa sababu ya kutimiza matakwa ya sheria ,ama kwa sabau kusikia na kuamini injili ?Je ninyi ni wajinga kiasi hicho?Ninyi mlianza kata msaada wa Roho .Je mnataka sasa kumaliza kwa nguvu zenu wenyewe ?….lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na sheria ,wako chini ya laana.

Wagalatia 5:1-4:-Basi simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya utumwa….Kama nikikubali kutahiriwa….Nasema tena wezi ,kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika sheria yote mmejitenga mbali na Kristo ,muko nje ya neema ya Mungu.

Wafilipi 3:8,9:-Naona kila kitu kuwa hasra tupu …Kwa ajili ya jambo bora zaidi yaani kuwa na Yesu kristo bwana wangu.Mimi sitaki tena uadilifu unaotokeana na kutii sheria sasa ninao uadilifu unaotokeana katika kumwamini Kristo ….uadilifu utokao kwa Mungu na ambao unategemea imani.

Wakolosai @:16-18;20-23:-Kwa hiyo basi msikubali masharti na mtu yeyote,kuhusu chakula ama vinywaji ,siku za sharehe ,sikuku ya mwezi mpya au sabato .mambo ya aina hiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja .Ukweli wenyewe ndiye Kristo …..Ya nini kuwekewa masharti ….Mshike hiki ,msionje kile msiguze kile .Mambo  hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa hayo ni mafundisho na maagizo ya ya kibinadamu tu.Kweli masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima  kwa namna ya ibada  wanayojishurutisha unyenyekevu na kutendea mwili kwa ukali.;lakini hayafai chochote kuzuia tama za mwili.

 

Angalia zaidi kwa:-  http://robertd128.sg-host.com/

 

MAANDIKO TAKATIFU MENGINE

Waroma 3:31,Wakolosai 3:4,1 Timothy 1:8-9,Yakobo 2:9-11

1.Hii ni tarakilishi iliyowazi yenye maelezo ya dondoo za vifungo vya kwanza na ya pili.

2.Angalia zaidi kwa  “HOW IS THE LAW FULFILLED”.

Let the Journey Begin - Bible study in Swahili!

Let the Journey Begin – Bible study in Swahili!